Botswana yakabiliwa na uhaba wa dawa

NOTSWANA : SERIKALI ya Botswana imetangaza hali ya dharura ya kiafya baada ya kuporomoka kwa mnyororo wa usambazaji wa bidhaa za matibabu nchini humo. Akilihutubia taifa hilo,Rais Duma Boko amesema hospitali nyingi zimekumbwa na uhaba mkubwa wa dawa muhimu, hali iliyolazimisha serikali kuchukua hatua za haraka.

Rais huyo alibainisha kuwa Wizara ya Fedha imeidhinisha bajeti ya dharura ya dola milioni 18.7 ili kushughulikia mzozo huo. Aidha, jeshi limetumwa kusimamia usambazaji wa dawa za dharura, ambapo shehena za kwanza ziliagizwa kuondoka mara moja kutoka mji mkuu wa Gaborone, zikipeleka msaada zaidi katika maeneo ya vijijini.

Tangu kuanza kwa mwezi huu, Wizara ya Afya imezielekeza hospitali kuahirisha huduma zisizo za lazima kutokana na uhaba wa dawa. Ripoti zinaonyesha kuwa hali hiyo imesababishwa na kupunguzwa kwa misaada ya maendeleo ya afya kutoka Marekani, pamoja na kuporomoka kwa mapato ya taifa kufuatia kudorora kwa biashara ya almasi duniani.

Botswana, yenye wakazi wapatao milioni 2.5, ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa almasi duniani, sekta inayochangia pakubwa uchumi wake. SOMA: Amnesty yaikosoa serikali ya Trump

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button