Bunge lapitisha Sh Trilioni 1.24 za Wizara ya Kilimo

DODOMA: BUNGE limeidhinisha jumla ya Sh 1 242, 975,000( Trilioni 1.242) kwa ajili ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Hili limekuja baada ya jana Mei 21, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwasilisha makadirio ya wizara hiyo pamoja na maeneo ya kimkakati waliyolenga kuyafanyia kazi.
Wabunge mbalimbali walitoa michango yao kwenye bajeti hiyo huku wengi wakipongeza kazi iliyofanywa na wizara na kuitaka wizara hiyo kufanya makubwa zaidi kutokana na ongezeko la bejeti ya wizara hiyo.
Akizungumza wakati akihitimisha hoja yake baada ya michango ya wabunge, Waziri Bashe amesema mipango ya wizara yake ni ya muda mrefu kwani wanafikiria pia kwaajili ya kizazi kijacho.
Bashe amesema tangu enzi za Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kilimo kilikuwa uti wa mgongo wa taifa ndio maana wizara yake imeyabeba maono hayo.
Naibu Spika wa Buge, Mussa Hassan Zungu ameitaka Wizara ya Kilimo kwenda kutekeleza yale waliyoahidi katika wasilisho lao la makadirio ya bajeti huku akilitaka bunge kwa ujumla kuwa mabalozi wa kuyasemea mazuri yaliyofanywa na Serikali.
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now, YOU can too with the Home Profit System:
ACT NOW➢ https://Www.Earnapp1.com