CBE yatakiwa kuanzisha kozi maalum za Elimu ya Biashara

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametoa wito kwa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzisha kozi maalum za muda mfupi na mrefu za Elimu ya Biashara.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Kitaaluma wa chuo hicho uliofanyika leo Novemba 12, 2025 jijini Dodoma, Prof. Nombo amesema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kuzalisha walimu wa kufundisha somo la Biashara, ambalo sasa ni la lazima kwa wanafunzi wote kwa mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, toleo la 2023.

Prof. Nombo amepongeza CBE kwa mafanikio ya kitaaluma, ikiwemo kushika nafasi ya nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu nchini kwa mujibu wa AD Scientific Index.

Amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha dhamira ya chuo katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya viwanda na biashara.

SOMA: CBE yashukuru mwitikio harambee mabweni ya wasichana

Aidha, ameeleza kuwa CBE imefanya tafiti 418 na kuchapisha machapisho 447 ndani ya miaka mitano, akisisitiza umuhimu wa matokeo hayo kufikishwa kwa wananchi kwa lugha rahisi na inayoeleweka huku akitoa rai kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuboresha miundombinu na kutoa mafunzo kwa wajasiriamali.

Amesisitiza kuwa vyuo vya elimu ya juu vina jukumu la kuhakikisha matokeo ya tafiti yanawafikia wananchi wa kawaida kwa lugha rahisi na inayoeleweka, ili kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii katika mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Ametoa rai kwa vyuo vingine nchini kuiga mfano wa CBE kwa kuandaa mikutano ya kitaaluma kama huo, kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuendeleza tafiti na kupanua wigo wa maarifa katika sekta mbalimbali.

Ameeleza kuwa tafiti ni kiini cha mageuzi ya Taifa, na ushirikiano kati ya vyuo, serikali na sekta binafsi ni muhimu ili kuhakikisha matokeo ya tafiti yanachochea maendeleo jumuishi.

Mkutano huo wa kitaaluma unajadili masuala muhimu yanayolenga kuimarisha ustahimilivu wa uchumi na biashara kwa maendeleo jumuishi.

Mada zilizotolewa zinahusu uchumi wa kimataifa, ujumuishaji wa kifedha, teknolojia na ubunifu, usimamizi wa mnyororo wa ugavi, soko la ajira, na siasa za kikanda na umehudhuriwa na viongozi wa serikali.

Habari Zifananazo

13 Comments

  1. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Duka Nitakuja kusoma

    1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Mahindi ya Kuchoma Nitakuja kusoma

  3. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Mahindi ya Kuchemsha Nitakuja kusoma

  4. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Mama Ntilie, Baba lishe, Mama lishe Nitakuja kusoma

  5. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Kuuza Miwa Nitakuja kusoma

  6. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Kuuza ticket za mabasi Nitakuja kusoma

  7. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Kuuza Bar Nitakuja kusoma mkianzisha hizo kozi

  8. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Mitumba Nitakuja kusoma mkianzisha hizo kozi

  9. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza kuendesha bodaboda Nitakuja kusoma mkianzisha hizo kozi

  10. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza kuendesha Guta Nitakuja kusoma mkianzisha hizo kozi

  11. Picha yako ya leo tutaitumia (kitabu cha mafanikio ya historia ya maisha yake imo) - MILEMBE University says:

    Nilichoka kuuza Kujenga Nyume Nitakuja kusoma mkianzisha hizo kozi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button