CCM kuanza 2025 na mrithi wa Kinana (3)

TUNAHITIMISHA safari yetu ya mfululizo wa makala kuhusu nafasi ya Makamu Mwenyekiti ndani ya Chama Cha Mapin duzi (CCM) upande wa Tanzania Bara.

Kama tulivyoona matoleo yaliyopita kuhusu majina mbalimbali yanayotajwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini kwamba pengine miongoni mwao linaweza kuwapo jina moja au lingine.

Inaweza kuwa pengine ni bahati nzuri au la, ni kwamba wiki tunayohitimi sha makala yetu ndiyo wiki ambayo CCM inafanya Mkutano Mkuu Maalumu jijini Dodoma, ambao utamchagua Makamu Mwenyekiti baada ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitisha jina lake.

Lakini siku hizo hizo mbili, ndizo ambazo miamba ya soka nchini Simba na Yanga, nazo zitakuwa zikipambania taifa katika michezo ya Afrika ngazi ya klabu.

Itaanza Yanga Jumamosi ikiikaribisha MC Alger kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na siku inayofuata Simba itakuwa uwanja huohuo kuikabili CS Constantine ya Algeria katika Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Nimechomekea ya miche zo pengine kwenye makala zilizopita sikuzungumzia kuhusu hilo, kwani pamoja na sifa nyingine michezo nayo ina nafasi yake kubwa katika uongozi.

Ni wazi makada waliota jwa matoleo ya nyuma akina Abdallah Bulembo, Mizengo Pinda, Steven Wasira kuwataja kwa uchache, wana nafasi yao kwenye masuala ya michezo.

Mfano, Bulembo amepata kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpi ra wa Miguu Tanzania (FAT) sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na pia kiongozi wa timu na vyama vya mpira wa miguu.

Hivyo CCM inayo hazina ya wanachama wake ambao wana sifa nyingi za uongozi ikiwamo hiyo ya ziada ambayo ni upenzi wa michezo.

Hivyo Makamu Mwe Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana. nyekiti mpya awe Pinda, Bulembo, Wasira, Anne Ma kinda au mwingine, anaweza kutumia turufu ya michezo kukinadi chama kwa wapiga kura.

Suala lingine ambalo hatukuligusia ni kipaji. Kila mtu aliyezaliwa anacho kitu cha pekee alichojaaliwa kuwa nacho.

Kitu hiki si umbile lake, elimu yake, umaarufu wake, usomi wake, cheo chake katika jamii, au utajiri wake wa vitu na fedha; la hasha, bali ni kipaji chake. Kipaji ni uwezo wa kiasili ulio ndani ya mtu katika mambile, nafsi na roho yake. Kipaji kinatoka ndani yake.

Ni tunu au zawadi toka kwa Mungu ambayo hakuna anayeweza kutunyang’anya au kutuibia mpaka tutaka pokufa.

Kipaji ni karama. Kwa kawaida kila mtu ameletwa duniani kwa ku sudi maalumu na la kipekee. Ili kutekeleza ku sudi hilo, Mungu katujaalia vipaji mbalimbali, wengine wamepewa vipaji vya uimbaji, uigizaji, ufundi, uchoraji, uchongaji, ususi, uchezaji muziki, uchek eshaji, uchezaji michezo mbalimbali, ujasiriamali, utabibu, ualimu, uongozi katika jamii, ugunduzi, uandishi na kadhalika.

Hivyo, haitarajiwi nafasi ya Makamu Mwe nyekiti CCM kupewa mtu wa kujifunza au kufanya majaribio, inatakiwa mwe nye kipaji cha uongozi.

Si nafasi ya kujifunzia na kwa ukubwa na uko mavu wa CCM, itapendeza zaidi Makamu Mwenyekiti mpya akafanana na waliomtangulia.

Afanane na akina Mzee John Malecela, Mzee Pius Msekwa, Mzee Philip Mangula, na Komredi Abdulrahman Kinana katika kukabili siasa za ushin dani wa vyama vingi na kudhibiti makundi ndani ya CCM hasa kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Makamu wenyeviti niliowataja awali, kila mmoja na haiba yake, lakini wote wanafanana kwa uwezo, hekima na busara katika kushughulikia masuala ya siasa hasa ya chama tawala.

CCM wanahitaji Makamu Mwenyekiti msemaji, mwenye mvuto, ushawishi wa makundi na rika tofauti, mtu mkweli na asiyeyumbishwa kwa maslahi binafsi au ya kikundi.

Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM ni lazima awe na mtaji binafsi wa kumuongezea kura mgombea urais wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Je, ni Komredi Bulembo, Pinda, Wasira, Anne Makinda au ni kada yupi kati ya wale tuliowagusia siku za nyuma?

Kwa upande mwingine, CCM wanahitaji Makamu Mwenyekiti licha ya kuwa ni wa Tanzania Bara, lakini mwenye kukubalika Tanzania nzima ikiwamo Tanzania Zanzibar.

Wakati huu ambao wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wanajian daa kwa safari ya kwenda Dodoma, ni muhimu sana wakumbuke kuwa siasa ni shughuli ya makundi, mwanasiasa asiye na kundi hawezi kukisaidia au kumudu mikikimikiki ya siasa.

Makamu Mwenyekiti mpya atakayepatikana anahitajika mtu mwenye ushawishi na mwenye watu ambaye hatolazimika kuanza kujitambulisha kwa umma.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba alikumbana na mgombea ubunge ambaye hata mwenyekiti wake wa chama hamjui.

Habari Zifananazo

Back to top button