CCM kuanza 2025 na mrithi wa Kinana(2)

DAR ES SALAAM; WIKI iliyopita tulianza makala haya kwa uchambuzi wa kada wa siku nyingi, Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi na mbunge, Abdallah Bulembo.
Kwa wale ambao hawakubahatika kusoma uchambuzi wa wiki iliyopita ni kuwa, Komredi Bulembo mwenye umri wa miaka 63, bado anabeba matumaini ya zama za sasa kama kuna mwanasiasa ndani ya CCM atakayeimudu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara ni kada mwaminifu na mtiifu, mzalendo na ambaye wakati wote yupo tayari kwa utumishi wa chama kuhakikisha ushindi unapatikana.

Kwa nini nasema hivyo? Kama mnavyofahamu Bulembo hajapitwa na wakati. Ikiwa zama za leo ni za vijana na watu wa umri wa kati.
Wapigakura wengi ni vijana na hadhira ya kisiasa imebadilika sana, hivyo ana hitajika makamu mwe nyekiti wa CCM anayeweza kuyanadi matarajio ya vijana katika ulingo wa kisiasa na zaidi kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Anaonekana pia kuwa mwanafalsafa ambaye amegeuka kuwa tumaini la mabadiliko chanya ndani ya CCM.
Anao uwezo wa kusaidia CCM kukabili changamoto za kisiasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Bulembo ni mtu mwe nye misimamo isiyoyumba kitakachoamuliwa iwe na kikao au maazimio yoyote ya mustakabali wa chama ndicho atakachokisimamia.
Bulembo hakengeuki, ni mtu ambaye habadiliki kama kinyonga katika jambo mlilokubaliana, lakini pia hana sifa ya ‘joka la mdimu.’ Si kigeugeu na si ndumilaku wili.

Sasa tumtazame Komredi Mizengo Pinda ambaye ana umri wa miaka 78. Ni Waziri Mkuu mstaafu na kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Pinda ni mtumishi wa muda mrefu serikalini.
Kilele cha mafanikio yake katika safari ya kisiasa ilifikia pale Februari 9, 2008 alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kutokana na kujiuzulu kwa Edward Lowassa.
Pinda amehudumu katika wadhifa huo hadi Novemba 5, 2015 alipostaafu. Kuhusu msimamo wake kwa chama, hauna mashaka, Pinda hatafuni maneno, nyeusi atasema nyeusi kamwe hawezi kusema nyeupe.
Kutokana na hulka hiyo, baadhi ya watu wanamtazama kama mhafidhina kwa matamshi yake, lakini kwake yeye muhimu kusimamia ukweli kama ahadi ya Mwana CCM inavyosema, “Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko”.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanachukulia hali hiyo kama changamoto ita kayomkabili na wanadhani haitaweza kumsaidia ikiwa atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Changamoto nyingine ambayo inaweza kuwa kikwazo kwake ni umri wake kuwa sasa umeenda, umri umemtupa mkono. Siasa zinahitaji nguvu huku hadhira ya kisiasa kwa sehemu kubwa ni ya vijana. Vijana wana mambo yao, matumaini yao ni kuona kiongozi anayebeba ‘kesho yao’ katika ulimwengu unaoendelea kwa kasi kubwa huku teknolojia ikichukua mkondo wake kwa vijana.
Kada mwingine anayetajwa kuweza kumrithi Komredi Abdulrahman Kinana mwezi huu ni Komredi Stephen Wasira mwenye umri wa miaka 80.
Wana CCM wengi wanamuona kama mwa nasiasa aliyezeeka na ambaye hawezi tena kuhimili mikikimiki ya kisasa hasa siasa za kwenye majukwaa ambazo kwa sehemu kubwa, ndizo zinazotumika kukinadi chama cha siasa kwa wapigakura.
Mzee Wasira ameanza kutumikia katika uongozi enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Katika hali ya siasa ya wakati tulio nao, Wasira hakuna wa rika lake, wengi wanamuona babu na baba.
Katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1995, Mzee Wasira aligombea kuteuliwa na CCM kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Bunda, lakini alishindwa katika kura za maoni ndani ya CCM baada ya wana CCM kumchagua Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu. Mzee Wasira, hakuridhika na ushindi wa Jaji Warioba, alihamaki na kuamua kuhama CCM akajiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi na kuamua kushindana na CCM katika Jimbo la Bunda ambako alishinda dhidi ya mgombea wa CCM, Jaji Warioba.
CCM kupitia mgombea wake, Jaji Warioba ilipinga matokeo hayo mahakamani ambako Mahakama Kuu Mwanza ilitengua ubunge wa Mzee Wasira mwaka 1996.
Katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwaka 1999 katika Jimbo la Bunda, Mzee Wasira tayari alishaihama NCCR Mageuzi na kumpigia debe mgombea wa Chama cha UDP, Victor Kubini. Baada ya uchaguzi huo, Mzee Wasira alijiunga tena na CCM.
Uchaguzi wa mwaka 2005 alijitosa Jimbo la Bunda na alishinda kura za maoni ndani ya CCM na kuwa mgombea katika jimbo hilo ambako katika Uchaguzi Mkuu alipita bila kupingwa, akatangazwa kuwa mbunge.
Baraza jipya la Mawaziri likaundwa Januari, 2006, Mzee Wasira aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji. Mwanasiasa huyu amekuwa na kauli tata na kutotabirika katika ua muzi, ukitazama historia yake kisiasa.
Komredi Mzee Wasira, umri mkubwa unam zonga, kwa karne hii ya vijana kushika hatamu za uongozi, anaonekana kuwa ‘babu’ na kustahili kupumzika. Itaendelea wiki ijayo



