CCM kuendesha harambee kusaidia kampeni

DAR ES SALAAM; CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kitaendesha harambee maalumu kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kampeni za chama hicho wenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Katibu Mkuu wa CCM amabye pia ni mgombea mwenza wa urais kwenye uchaguzi huo Dk Emmanuel Nchimbi amesema harambee iyo itazinduliwa kesho Agosti 12, 2025 jijini Dar es Salaam na dhamira ni kupata Sh bilioni 100.



