CCM kuzingatia mgawanyo walimu sekondari Kahasa

MWANZA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amesema atahakikisha mgawanyo wa walimu unazingatia Shule ya Sekondari Kahasa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata walimu wa kutosha na mazingira bora ya kujifunza.

Kihongosi ameeleza hayo leo Machi 12,2026 alipotembelea na kukagua mradi huo wa shule uliopo katika Kata ya Ilemela Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza , ikiwa anahitimisha ziara yake katika mikoa ha kanda ya ziwa.

Kihongosi amesema hayo akifafanua taarifa ya Mkuu wa shule iliyosomwa mbele yake ambayo ilikuwa ikieleza kuwa shule hiyo ina walimu 13 pekee, akieleza hilo amesema pamoja na upya wa shule hiyo lakini imeendelea kufanya kazi lakini inahiitaji ongezeko la walimu, hivyo atahakikisha serikali inapofanya mgawanyo wa walimu mashuleni wanafika na hapo.

Kihongosi amesema ni jambo zuri na la faraja kuona Halmashauri zinatumia mapato ya ndani kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, huku akipongeza wazazi kuruhusu watoto wao kwenda shule kusoma kwa sababu kuna wazazi wengine ambao hawapeleki watoto shule.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa shule, Oliver Kimathi imeelezwa ujenzi wa shule hiyo mpya katika Wilaya ya Ilemela unalenga kupanua fursa za elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo ambao hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata masomo ya sekondari.

Amesema mradi wa ujenzi wa shule hiyo ulianza Januari 18, 2025 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela na hadi sasa utekelezaji wake umefikia takribani asilimia 68.5.

Kimathi amesema jumla ya Sh milioni 584 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo, ambapo hadi sasa kiasi cha sh. milioni 400 tayari kimetumika kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya madarasa, maabara za sayansi, jengo la utawala, maktaba pamoja na matundu ya vyoo kwa wanafunzi na walimu.

Amesema tayari shule hiyo imesajili wanafunzi 358 ambapo kidato cha kwanza ni wanafunzi 185 na kidato cha pili ni 171 wanaoendelea na masomo, hivyo ni muhimu kuongeza idadi ya walimu ili kuendana na ongezeko hilo na kuwasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao za kielimu.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za jirani, kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea kwenda shule na kuongeza nafasi za wanafunzi kuendelea na elimu ya sekondari katika Kata la Ilemela.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button