CCM yapokea mapendekezo ya Azaki kuhusu upoteaji, utekaji

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimepokea mapendekezo kutoka kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) zaidi ya 300 nchini, yanayopendekeza kuundwa kwa tume huru ya kiraia kuchunguza matukio ya utekaji na upoteaji wa watu, pamoja na serikali kusaini mikataba ya kimataifa ya kulinda watu.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa jijini Dar es Salaam na Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, na kupokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella.

Olengurumwa amesema lengo la mapendekezo hayo ni kuwasilisha hoja muhimu zinazohitaji hatua za haraka kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Amesema hoja hizo ni pamoja na kukomesha vitendo vya utekaji na upoteaji wa watu, kulinda uhuru wa vyombo vya habari na Asasi za Kiraia, kuhakikisha mazungumzo ya kitaifa yanafanyika kwa ajili ya maridhiano, na kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya kwa ushirikiano mpana wa wananchi.

SOMA ZAIDI: CCM yampongeza Samia ukemeaji utekaji

Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2023 hadi 2025, matukio zaidi ya 100 ya utekaji na upoteaji wa watu yameripotiwa nchini, yakihusisha watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari na wanasiasa.

Aidha, AZAKI hizo zimeitaka serikali kuunda tume huru ya kiraia kuchunguza matukio hayo, pamoja na kusaini mikataba ya kimataifa ya kulinda watu dhidi ya kupotezwa kwa kulazimishwa. Pia zimeitaka serikali kuimarisha mazingira huru ya kisiasa na kijamii ili kuruhusu Asasi za Kiraia, vyombo vya habari na vyama vya siasa kufanya kazi bila hofu, sambamba na kurejesha imani ya wananchi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella, amesema chama hicho kinatambua mchango wa Asasi za Kiraia katika kuimarisha demokrasia, haki za binadamu na utawala bora nchini. Amesema CCM itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha hoja zinazowasilishwa na AZAKI zinachukuliwa kama fursa ya kujenga taifa lenye umoja, amani na haki sawa kwa wote.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    THIS→→→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button