CCM yampongeza Samia ukemeaji utekaji
DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake aliyoitoa mkoani Kilimanjaro ya kukemea vitendo vya utekaji na mauaji huku akiliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini wanaohusika na vitendo hivyo.
Pia chama hicho kinalaani vikali vitendo vya upotoshaji wa hotuba hiyo vinavyofanywa na wapinzani hususan Chadema.
Hayo yameelezwa leo Septemba 21,2024 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Chama Mapinduzi Taifa(CCM-NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makalla amesema Rais Samia alizungumza na kutoa kauli hiyo akiwa kama rais, kiongozi mkuu wa nchi na kama amiri jeshi mkuu lakini watu wenye nia mbaya wamekuwa mitandao na wengine katika vikao vyao wamekuwa wakipotosha na kulipa maana nyingine.
“Nataka niseme mheshimiwa Rais Baada ya taarifa za kifo Cha Kibao, alitoa pole na kutoa maagizo ya kufanyika uchunguzi Kwa kina, alitoa pole Kwa masikitiko makubwa tofauti na wengine wanavyo potosha kauli na maagizo ya Rais Dk.Samia,” amesema Makalla.
Aliongeza: “CCm kupitia Mwenezi nilitoa pole na siku hiyo Rais alitoa pole na maelekezo ya uchunguzi wa kina, kwa kusikitishwa na kifo hicho, vivyo kwa Rais na Watanzania wote Kila mmoja hili jambo lilimshtua, na alitaka lisijirudjie tena, inapotokeq jambo la kifo, wote linatusikitishaa.”
SOMA: Makalla akabidhi ofisi
Amesema baada ya hotuba Ile kumekuwepo upotoshaji na kauli zingine ambazo hazina maana kwa hiki tuweke wazi Rais Samia ametaka lichunguzwe.
Amesema upinzani kupitia mwenyekiti wao wamekuwa wakitoka kauli tofauti za kutokubaliana na uchunguzi ambao rais ameamuru ufanyike.
Pia amesema kuna mikakati ya Chadema ya kuchafua nchi, hawapendezwi na amani na maendeleo makubwa yaliyopo na yanayoendelea kufanyika nchi nzima.
SOMA: Serikali yatoa tamko matukio utekaji
Amesema linalo wapa shida Chadema ni utendaji mkubwa wa Rais Dk.Samia na kupeleka fedha nyingi vijijini kuliko awamu nyingine, miradi mikubwa imeendelea kutekelezwa, ikiwemo Bwawa la Mwalimu lililojengwa, Reli ya Kisasa, mradi wa kununua ndege ambazo wanazitumia.
Sambamba na hayo amesema CCM imejipanga vizuri kushinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia ya kutekeleza miradi mikubwa na kupeleka fedha nyingi vijijini za utekelezaji miradi ya maendeleo.
BALOZI NCHIMBI ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo ameshiriki kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza Kuu.
Kikao hicho kiliongozwa na… pic.twitter.com/yHqpSeqtZI
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) September 17, 2024