CCM yataka viwanda vichangie 25% pato Z’bar

ZANZIBAR: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaielekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) iongeze mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa kutoka asilimia 20.8 hadi asilimia 25. Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2022-2050 imeeleza viwanda ni sekta muhimu katika kukuza uchumi, kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kuleta ajira kwa wananchi.

CCM imeeleza kwamba itaielekeza SMZ iendeleze maeneo maalumu ya viwanda na kuwawezesha wazalishaji wadogo kutumia maeneo hayo. Pia, SMZ itaelekezwa iendeleze maeneo maalumu ya uwekezaji wa viwanda ikijumuisha maeneo ya Chamanangwe Pemba na Dunga Unguja kwa kuweka miundombinu ya uzalishaji. Ilani inataka SMZ iweke mkakati wa kuanzisha viwanda vipya kupunguza uingizaji wa bidhaa kutoka nje kwa bidhaa maalumu na kukidhi asilimia 60 ya mahitaji ya ndani.

CCM inataka SMZ iandae mfuko maalumu wa kukuza viwanda vidogo na iweke vivutio vya kodi kwa lengo la kuchochea uzalishaji wa bidhaa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. Ilani inaeleza CCM itaagiza kuimarisha mfuko wa maendeleo ya viwanda kusaidia viwanda vya kimkakati na pia SMZ iandae programu ya kukuza viwanda vya usindikaji wa bidhaa zinazotokana na mazao yenye thamani ikijumuisha viungo, mafuta ya mimea na mwani.

SOMA: ZEC yataka kampeni za kistarabu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button