“Chagueni wenye kasi ya Rais Samia”

SERIKALI ya Mkoa wa Mtwara imewataka wanawake wa Wilaya ya Mtwara mkoani humo kuacha majaribio katika uchanguzi wa Serikali za Mitaa badala yake wachague viongozi wenye uhakika watakaoendeleza kasi ya Rasi Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa wakati wa mafunzo ya siku moja kwa makundi mbalimbali ya wanawake na wanawake wajasiliamali kutoka katika wilaya hiyo, yaliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na kufanyikia katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo.

Lengo la mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuyajengea uwezo makundi hayo kuhusu masuala hayo ya ujasiliamali lakini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amesema hawatakiwi kurudi nyuma kwani Rais huyo ameufungua mkoa huo kupitia uwekezaji mbalimbali kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Mtwara tusiende kufanya majaribio nendeni mkachague kiongozi ambaye mna uhakika ataendeleza hii kasi ya mheshimiwa Rais wetu mkoa wetu uzidi kupaa, “amesema Sawala.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Abdallah Mwaipaya amesema wanapoelekea kwenye uchaguzi huo wameoona ipo haja ya kukutana na makundi hayo ili waweze kufurahi pamoja  na akina mama hayo na kupeana elimu kuhusu masuala mbalimbali yanaohusu maendeleo wilaya na mkoa kwa ujumla.

Ameyapongeza makundi hayo kwa umoja waliyouonyesha bila kujali itikadi za vyama vyao:”leo tumeawaita hapa tumeona mwitikio ulivyokuwa mkubwa kwa umoja wetu tunawashukuru sana”

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala mkoani humo, Thabitha Kirangi amesema kwa sasa zoezi linaloendelea kwenye ngazi ya jamii ni mikutano ya namna ya kuweza kufikia mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Kwahiyo akina mama, vijana na watu wenye ulemavu tusiikose fursa hii, mama amefanya upendeleo kwahiyo wakati unapoenda kujiandikisha nenda kasikilize na fursa nyingine”amesema Kirangi.

Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani  mkoani humo, Shadida Ndile amesema wanawake wa mtwara wana imana kubwa na serikali yao kwani wamejipanga vizuri na watayafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatolewa katika mafunzo hayo.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi hao wa vyama vya siasa ikiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mtwara mjini, Victoria Tungu  amepongeza jitahada zilizofanywa na viongozi wilayani humo kuwakutanisha wanawake hao na kuahidi kuendelea kudumisha umoja huo ili wazidi kuijenga mtwara yao.

Habari Zifananazo

Back to top button