Chalamila ataja matukio yaliyotikisa Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuna matukio matatu makubwa yaliyozua taharuki, 2024 likiwemo la bwana harusi Vincent Peter Masawe mkazi wa Kigamboni aliyedaiwa kurejea na baadae kugundulika kuwa alijificha mwenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya mkoa huo Chalamila amesema kuna matukio yameathiri mkoa huo kwa namna tofauti, lakini juhudi za pamoja za serikali na wananchi zimechangia kutatua changamoto hizo.

“Alijificha kutokana na madeni yaliyokuwa yakimkabili kutoka katika kampuni za benki na watu mbalimbali ambaye jeshi la polisi lilifanikiwa kumpata alikukuwa amejificha.”amesema

Advertisement

Chalamila ameeleza “Tukio lililoibua hofu kubwa, ambapo mtoto mdogo alipotea na kuhisiwa kutekwa na uchunguzi wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwa mtoto huyo alikuwa ametumbukia ndani ya kisima cha maji, amesema Chalamila.

Pia ameongeza kwa kutolea ufafanuzi tukio la mfanya biashara aliyejulikana kwa jina la Daisle Ulomi mfanya biashara wa Sinza ambaye alidaiwa kutekwa na kuuawa.

Chalamila amesema kuwa “Ulomi hakutekwa bali alipata ajali ya pikipiki na kusaidiwa na wasamalia kupelekea Hospitali ambapo alifariki na kutokana na kuwa hakuwa na kitambulisho chochote ilikuwa vigumu kuwapata ndugu zake hivyo mwili ukawekwa Katika chumba Cha kuhifadhia maiti Katika Hospitali ya Mwananyamala

“Kuna watu wakauliza kwanini apelekwe Hospitali bila polisi kupewa taarifa? Jeshi la Polisi limeelekeza kuwa majeruhi wanapaswa kupatiwa matibabu haraka bila kuhitaji fomu ya PF3, ili kuokoa maisha, Ni muhimu wananchi kuelewa kuwa utaratibu huu unalenga kuokoa maisha ya majeruhi, na sio kuwachelewesha kwa sababu ya taratibu za nyaraka,” amesema.

Aidha amesema sakata la kutekwa Kwa Abdul Nondo na kifo cha Ally Kibao Chalamila amebainisha kuwa taarifa za kutekwa kwake zilileta mkanganyiko, baada ya watu waliodhaniwa kuwa polisi kutumia pingu wakati wa tukio.

Amesema maafisa wa polisi wameagizwa kuhakikisha wanavaa sare rasmi wanapotekeleza majukumu yao ili kuepusha mkanganyiko na lawama zisizo za msingi.

Ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanatembea na vitambulisho vya taifa (NIDA) ili kurahisisha utambuzi na kusaidia mamlaka wanapokutana na changamoto.

“Kutokuwa na kitambulisho mara nyingi kunaleta changamoto katika kuwasaidia wananchi wanapopatwa na matatizo. Ni vyema kila mmoja ajitahidi kuwa nacho,” amesema Chalamila