Chalamila ataka kasi ujenzi BRT

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amempa wiki mbili mkandarasi kampuni ya CGC anayetekeleza ujenzi wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Nne kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Posta – Mwenge hadi ubungo, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia ucheleweshaji usio na sababu za msingi.
Chalamila amesema hayo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi ya maendeleo wilaya ya kinondoni ambapo amepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi kutoka kwa mkandarasi, mshauri wa mradi na Meneja wa Mradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Amesema mradi huo ni muhimu kwa jiji la Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia kupunguza msongamano wa magari na kuboresha huduma ya usafiri kwa wananchi, hivyo utekelezaji wake unapaswa kukamilika kwa ubora na kwa muda uliopangwa.

“Nataka kazi ifanyike saa 24, mchana na usiku. Sitamchekea mkandarasi yeyote, barabara lazima ikamilike,” amesema Chalamila.
Amesema ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo kwa baadhi ya maeneo unatokana na vitendo vya uzembe na changamoto ya rushwa kwa baadhi ya viongozi, huku akisisitiza kuwa lazima kuwe na uwajibikaji ili miradi ya wananchi ikamilike kwa wakati.
“Nataka kufahamu commitment level ya mkandarasi. Serikali imetoa fedha, wananchi wanahitaji huduma, hatuwezi kuchelewa bila sababu,” amesema.
Kwa mujibu wa Meneja msaidizi TANROADS Mhandisi Justine Moshi, mradi huo unaotekelezwa chini ya BRT Awamu ya Nne (LOT 1) unaohusisha eneo la Posta hadi Mwenge na Mwenge hadi Ubungo, ulisainiwa Juni 30, 2023 na ulitarajiwa kukamilika Machi 20, 2025, lakini muda wa kukabidhi mradi umeongezwa hadi Juni 15, 2026.
Amesema gharama ya mradi ni Sh bilioni 174.38, huku mkandarasi akiwa tayari amelipwa Sh bilioni 51.1.
Ameeleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 47, wakati mpango ulionyesha mradi huo ungetakiwa kuwa umefikia asilimia 65.
Naye mshauri elekezi (consultant) wa mradi amesema changamoto kubwa inayoikabili kampuni inayotekeleza mradi huo ni kuchelewa kwa uhamasishaji wa vifaa vya ujenzi (mobilisation of equipment), hali inayosababisha kazi kutofanyika kwa kasi inayotakiwa.

Chalamila amesisitiza kuwa madai ya baadhi ya wakandarasi kuwa utekelezaji wa miradi mijini ni mgumu kuliko maeneo ya vijijini hayana msingi, na kwamba sheria na taratibu za TANROADS zipo wazi hivyo mkandarasi anatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji mara moja.
Amesema atarejea tena baada ya wiki mbili kufanya ukaguzi wa mradi huo ili kujiridhisha kama hatua zilizochukuliwa zimeleta mabadiliko yanayoonekana.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa inaendelea katika maeneo mbali mbali Mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya kinondoni kwa lengo la kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com