Chalamila: TRA toeni elimu kwa mlipa kodi

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya oparesheni maalum ya elimu kwa mlipa kodi nchini ili kusaidia kukusanya mapato kwa kiwango kikubwa.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha kuhamasisha ulipaji kodi awamu ya nne na kubainisha  kuwa miongoni mwa vitu vinavyoiongoza nchi ni ukusanyaji kodi kwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa.

Advertisement

 

Awali akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TRA Edmund Kawamala Naibu kamishna kodi za ndani divisheni ya walipa kodi wadogo  amesema makusanyo ya kodi nchini yanategemea Mkoa wa Dar es salaam maana ndio mkoa wa kitivo cha biashara na walipa kodi wengi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule amesema wataendelea kushirikiana na TRA  kwa karibu katika Wilaya hiyo ili waweze kuwafikia walipa kodi na  kukusanya mapato ya Serikali kikamilifu.

1 comments

Comments are closed.