Chama Tawala chaongozo Moldova

MOLDOVA : CHAMA tawala cha Moldova kinachounga mkono Umoja wa Ulaya (EU) kimeibuka kinachoongoza katika uchaguzi wa bunge, kufuatia kura zilizohesabiwa mapema jana.Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa baada ya kuhesabiwa kwa zaidi ya asilimia 95 ya kura, Chama cha Action and Solidarity (PAS) kilichoko madarakani tangu mwaka 2021, kimepata asilimia 48.3, huku Kambi ya Patriotic inayoshirikiana na Urusi ikipata asilimia 25.5.
Uchaguzi huo, uliofanyika Jumapili, umeelezwa kuwa muhimu kwa mustakabali wa taifa hilo dogo linalopakana na Ukraine, kutokana na msukumo wake wa kujiunga na EU baada ya Urusi kuivamia Ukraine mwaka 2022.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button