Moldova kujiunga EU bado kitendawili

MOLDOVA : KURA ya maoni iliyopigwa nchini Moldova ya mabadiliko ya katiba haijaonyesha ushindi wa kuruhusu nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya .

Mpaka sasa kura zilizopigwa zinaonyesha kuna mgawnayiko mkubwa wa kura za ndio au hapana ambazo zinaenda sambamba huku zikisalia kura asilimia 2% tu kuhesabiwa

Katika kura hizo upande wanaounga mkono wamepata kura asilimia  50.18 na upande unaopinga wamepata asilimia 49.92.

Advertisement

Mpaka sasa zaidi ya asilimia 98 ya kura zimeshahesabiwa kulingana na utafiti wa maoni uliofanywa na kuonyesha kura zilizounga mkono hoja ya Moldova kujiunga na umoja wa ulaya zilikuwa zinaongoza.

Naye Rais wa nchi hiyo,Maia Sandu amesema hajaridhishwa juu ya matokeo hayo kutokana na kile alichokiita kuwa ni uingiliaji wa nchi za nje.

SOMA : Mpango wa Zelensky kutangazwa