Mpango wa Zelensky kutangazwa

BRUSSELS : RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amepanga kuwasilisha mpango  wa ushindi kwa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami NATO mjini Brussels hii leo.

Mpango huo utakwenda sambamba na ombi la kujiunga uanachama wa NATO na ongezeko la msaada wa kijeshi katika kampeni zake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Mpango wa Zelenskiy unajumuisha maombi ambayo washirika wa Ukraine hadi sasa wamekataa kuyakubali, kama vile wito wa kualikwa kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO na ruhusa ya kutumia silaha za Magharibi kushambulia ndani ya Urusi.

Advertisement

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte amesema  wanachama 32 wa jumuiya hiyo wataupitia mpango huo na kuusoma kuweza kuuelewa ili waweze kuyatolea maamuzi.

SOMA: Waliopanga kumuua Zelensky wakamatwa