‘Changamoto 22 Muungano zimepatiwa ufumbuzi’

DODOMA; SERIKALI imesema jumla ya changamoto 22 za Muungano zimepatiwa ufumbuzi.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mwera, Zahor Mohammed Haji aliyehoji ni lini serikali itapeleka muswada wa sheria kuhusu changamoto za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi, ili ziwe kwa mujibu wa sheria.
“Nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa mpaka sasa jumla ya changamoto 22 za Muungano zimekwishapatiwa ufumbuzi.
“Aidha, katika kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 4 Aprili, 2025 Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Muungano kilitoa maelekezo kwa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa SJMT na SMZ kufanyia kazi jambo hilo.
“Aidha, mara baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha taarifa ya utekelezaji taarifa itatolewa kwa umma,” amesema Naibu Waziri.