Chanzo cha moto Kariakoo ni hujuma-Chalamila

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema chanzo cha moto Kariakoo ni hujuma iliyofanywa na wafanyabiashara wenyewe na si ajali.

Chalamila ameyasema hayo leo Oktoba 20, 2023 akielezea majibu ya ripoti ya kamati ndogo aliyoiunda baada ya moto kuibuka hivi karibuni katika eneo la mnadani Kariakoo na kuteketeza baadhi ya majengo, maduka na vibanda vya wafanyabiashara.

Akizungumza Chalamila amesema “Oktoba Mosi, moto mkubwa uliteketeza maduka na vibanda kadhaa vya wafanyabiashara Kariakoo na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.

“Hata hivyo, baada ya tukio hilo niliunda kamati ya watu zaidi ya saba ya kuchunguza ikihusisha vyombo vya ulinzi na usalama, kamati imeshakamilisha uchunguzi wa awali na kubaini kuwa moto ule ni hujuma na si ajali ya bahati mbaya.”Amesema Chalamila

Amesema, mgogoro baina ya wafanyabishara wa mnadani Kariakoo na uongozi uliopo ndio umesababisha kuhujumiana.

“Maelezo ya waliohojiwa wafanyabiashara na walinzi wa mnadani yalionekana kuwa yamepangwa na hayaakisi uhalisia wa tukio husika pia namna moto ulivyoanza na kukua kwa kasi tumeangalia kupitia kamera za CCTV zilizopo pembezoni mwa moto ulikoanzia ,” amesema Chalamila.

Amesema, wafanyabiashara wa awali walisema moto huo umesababishwa na jenereta ambalo lilikua pembezoni mwa Kariakoo Auction Mart, kamati imegundua jenereta hilo ni zima na halikuungua na wala sio chanzo cha moto huo.

Chalamila amesema, Kamati imetoa ushauri na mapendekezo moja wafanyabishara wa vyuma chakavu kutafutiwa eneo mbadala, watoke kwenye eneo la sasa ambalo limeonyesha wazi kama utatokea tena moto madhara yake yatakua ni makubwa zaidi.

Pia, Halmashauri kusimamia sheria zinazoelekeza upangaji wa miji na majiji kwa majengo, kuacha njia za wazi za dharura baina ya jengo moja na jengo lingine, ilikama itatokea majanga mambo yasuluhishwe kirahisi.
Aidha, imependekeza pia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kufanya mapitio ya Kampuni ya Kariakoo Auction Mart ili kupata uhalali wa umiliki na namna ya uendeshaji wa kampuni hiyo na kama itabaini mpaka sasa hakuna wamiliki halali, eneo hilo litakua chini ya udhibiti wa serikali mpaka hapa watakapopata majibu mazuri ya kisheria.

“Nasisitiza pia sambamba na madhara yaliyotokea, ni wazi usiopingika wafanyabishara zaidi ya 550 walipata madhara katika maduka yao ambayo hatua za awali zinaonyesha walikuwepo wakati maduka yanashika moto
“Uchunguzi huu umehusisha eneo la tukio, kufanya mahojiano ya kina na mashuhuda , wamiliki wa majengo wafanyabiashara na walinzi wa zamu.

“Tumezichunguza kamera zote zinazozunguka eneo hilo ikiwemo benki ya Baroda na maeneo mengine kwa mantiki hiyo, navielekeza vyombo vyote vinavyoshugulika na masula ya uvunjifu wa sheria vianze kazi mara moja ili kuwabaini watu wote waliohusika, ripoti hii watapewa vyombo vya usalama kwa hatua za awali za kisheria.”Amesisitiza Chalamila.

Aidha, akizungumzia changamoto zilizojitokeza wakati wa kupambana na moto ikiwemo ukosefu wa msukumo wa maji ya kuzima moto eneo la Kariakoo siku ya tukio amesema changamoto ya upatikanaji wa maji, pamoja na uhaba wa maji katika visima vya maji ya kuzima moto na kubaini kuwa visima hivyo ni vichache kwa mkoa kwani havitoshelezi kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kumekuwepo na ujenzi holela eneo la Kariakoo Mnadani ambao haujahusisha uwekaji wa miundombinu wa njia za dharura pamoja na kuwepo kwa ujenzi uliyotumia mbao ambao imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa moto kwa kasi,” amesema.

“Eneo hilo pia lilihusisha uuzaji wa vifaa asilia ya vimiminika vinavyowaka na kulipuka ambavyo vinamgandamizo wa gesi pamoja na ucheleweshaji wa kutoa taarifa ya wito wa tukio la moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link… 

Try it, you won’t regret it!….. http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
JonelleMadoline
JonelleMadoline
1 month ago

I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, (r 08q) therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.
Just open the link——->> http://Www.SmartCareer1.com

Julia
Julia
1 month ago

I get paid more than $120 to $130 every hour for working on the web. I found out about this activity 3 months prior and subsequent to joining this I have earned effectively $15,000 from this without having internet working abilities.
.
.
Detail Here———————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

MaryShield
MaryShield
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by MaryShield
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x