Chelsea kulipa kisasi kwa Arsenal?

UINGEREZA: Wametafutana wee! hatimae wamekutana, wababe wa Epl kutoka Jiji la London Chelsea na Arsenal watavaana leo katika mchezo wa Epl utakaopigwa kuanzia saa moja na nusu usiku katika dimba la Stamford Bridge.
Mchezo huo ni wa nane kwa timu zote msimu huu kwenye Epl ambapo Arsenal inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na alama 20 wakati Chelsea ikishika nafasi ya 11 na alama 11.

Miamba hiyo ya London inaingia katika mchezo huo huku Arsenal wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 walioupata katika mchezo wa mwisho timu hizo zilipokuatana katika dimba la Emirates
Je nani kuwa mbabe wa Jiji la London leo?
3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *