KILIMANJARO: Msanii wa Bongo fleva nchini Isaya Mtambo, ‘Chino’ amesema kuwa hana ugomvi na msanii mwenzake Omary Mwanga ‘Marioo.
Chino amenukuliwa akisema wameshazimaliza tofauti zao sasa wako shwari kabisa.
Msanii huyo ametoa kauli hiyo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.
Chino amesema tofauti yao kubwa ilikuwa ni kuweka vitu moyoni wameshaambiana wameyamaliza.
“Sisi ni watoto wa kiume tulitakiwa kuongea na kuyamaliza tulishakaa tukaongea kubwa lilikuwa kutokuweka vitu moyoni tuliambiana tukayamaliza, kinachofuata saivi ni kufanya kazi kwa bidii hakuna bifu.”amesema Chino