Chongolo amuomba RC Makame kukamilisha bandari kavu Tunduma

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amemkabidhi Ofis Mkuu wa Mkoa mpya Jabir Makame katika ghafla fupi iliyofanyika leo Julai, 2 katika ukumbi wa ofis za mkoa, huku akimuomba kukamilisha ujenzi wa bandari kavu katika mpaka Tunduma ambao unaunganisha nchi za kusini mwa Afrika (SADC).

Akitoa neno fupi wakati akiaga Chongolo amesema mpaka wa Tunduma ambao unategemewa na nchi nyingi za kusini mwa Afrika utakuwa na tija kubwa zaidi pindi mradi mkubwa wa ujenzi wa bandari kavu ambao tayari maandalizi yalisha kamilika.

“Mpaka sasa tayari zaidi ya ekali 1800 zimelipiwa fidia kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Bandari hiyo kavu ambayo inategemewa kuwa na tija kubwa pamoja na kutengeneza fursa lukuki ikiwa ni pamoja na kupunguza foleni ya magari makubwa ya mizigo katika mpaka wa Tunduma,” amesema Chongolo.

SOMA ZAIDI

Chongolo ataka madeni ya wazabuni yalipwe Songwe

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa mpya Jabir Makame amesema akishirikiana na viongozi wengine atahakikisha anasimamia na kuendelea kukamilisha miradi yote ya kimkakati ukiwemo mradi wa ujenzi bandari kavu na kusimamia ukusanyaji mapato.

Katika tukio hilo pia limeambatana na makabidhiano ya ofisi kati ya katibu tawala mkoa anayeondoka Happness Seneda na katibu Tawala anayeingia ambaye ni Frank Hawas , sambamba na hilo pia Mkuu wa Mkoa amefanya uapisho kwa Mkuu mpya wa wilaya ya Songwe Fadhil Nkurlu .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button