Chuchu Hans ataja sababu za kushindwa kufunga ndoa

MWIGIZAJI maarufu wa filamu na tamthilia nchini Chuchu Hans, amesema uhusiano wake na mzazi mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’ sio tu haueleweki licha ya kuishi pamoja bali pia, kikwazo cha wao kushindwa kufunga ndoa ni suala la dini.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo Juni 5 amesema utofauti wa dini yeye muislam na mwenzake mkristo ni miongoni mwa mambo yanayoleta mvutano.

Amesema hajui ni lini watafunga ndoa, wanaendelea kuishi pamoja akiwa njiapanda na mzazi mwenzake kwani hana mpango wa kuanzisha mahusiano mapya kwa sasa.

“Nimekuwa kwenye mahusiano zaidi ya miaka kumi. Siri ya kudumu ni kujitambua na kujenga msingi imara wa maisha. Lakini ukiona mtu hashiki mkono wako kwenda mbele, ni lazima ujitathmini,” amesema.

Chuchu leo amesaini mkataba wa miaka mitatu wa ubalozi wa kampuni ya ujenzi ya Ligae.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button