‘Chupa ni mali zihifadhi, usizitupe’

DAR ES SALAAM; WATANZANIA wametakiwa kutunza mazingira na kuacha tabia ya kutupa chupa za plastiki ovyo, kwani zinaathiri maisha ya viumbe hai majini na nchi kavu.

Akizungumza HabariLEO, jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mjumuiko wa kampuni nane za uzalishaji wanaotumia chupa, PETPro Tanzania, Nicholous Abwene amesema Watanzania wanatakiwa kuweka vizuri mazingira kwa kutunza chupa za plastiki za maji, soda na juisi kwani ni malighafi inayoweza kuwaingizia kipato pia.

Advertisement

“Mambo mengi yanafanyika tunatamani yaende kwenye jamii ijue umuhimu wa chupa hizi na si kuzitupa bali kuhifadhi mazingira kwa kila mmoja wetu,” amesema.

 

Akizungumzia namna chupa zinavyochambuliwa, amesema kuwa kazi iliyopo kiwandani ni kutenganishwa zenye rangi na zisizo na rangi na kuondolewa mifuniko na nembo, baada ya hapo zinaingizwa kwenye mashine na kuchakatwa hadi zinapatikana bidhaa zingine.

Soma: Wabuni boti ya plastiki, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Amesema kuwa malighafi zinazopatikana ni kama mikanda ya kufungia vitu, pamba za kutengenezea mito na vitu vingine vingi.

Hata hivyo, mmoja kwa wakusanya chupa jijini Dar es Salaam, Juma Hamis amesema bado kuna unyanyapaa, kwani baadhi ya watu huwafananisha na wasio na akili timamu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

“Unakuta mtu ametumia chupa baada ya kuweka vizuri anatupa kwenye mfereji, wakati kama angeweka kwenye sehemu nzuri tungepita na kuchukua chupa safi,”  anasema Juma.