Wabuni boti ya plastiki, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

UNGUJA, Zanzibar: BOTI ya chupa za plastiki ni moja ya kivutio kinachopatikana ndani ya Kisiwa cha Unguja, Zanzibar.

Boti hii, hutumika kuhifadhia taka za plastiki kama bilauri na chupa za maji, maalumu kwaajili ya utunzaji wa mazingira na jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inayopelekea ongezeko la joto duniani.

Kituo cha Zanzibar ni kati ya vituo vitano vilivyoorodheshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwa na kiasi cha juu cha ongezeko la joto nchini kwa mwaka 2023.

“Hadi kufikia Disemba 29, 2023 kituo cha Zanzibar kiliripoti nyuzi joto 33.4 °C mnamo tarehe 02 Disemba, 2023 (ongezeko la nyuzi joto 1.6).” Imeeleza taarifa ya TMA.

Vituo vingine ni Morogoro, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam. Shughuli za binadamu hutajwa kuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira unaopelekea mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto.

Sababu nyingine ni kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua unaojitokeza katika maeneo mbalimbali.

Wastani wa ongezeko la joto la dunia katika mwaka wa 2023 ulifikia nyuzi joto 1.40C na ulivunja rekodi na kuwa ni mwaka wenye joto zaidi katika historia ya dunia, ukichagizwa na uwepo wa El Niño na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wa Tanzania, tathmini zinaonesha pia wastani wa ongezeko la joto kwa mwaka 2023 ulikuwa nyuzi joto 1.00C kwa upande wa Tanzania na pia kuufanya mwaka 2023 kuvunja rekodi na kuwa mwaka wenye joto zaidi katika historia.

Hakika, kongole Zanzibar kwa ubunifu huu wa boti ya chupa za plastiki kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi onayopelekea ongezeko la joto ulimwenguni.

Habari Zifananazo

Back to top button