Coco Gauff ampa ‘thank you’ kocha wake
Mcheza tenisi namba sita duniani kutoka Marekani, Coco Gauff, ameachana na kocha wake Brad Gilbert wiki mbili tu baada ya kile alichokitaja kuwa kampeni ya kukatisha tamaa kutetea taji la US Open.
Gauff, 20, alishinda taji lake la kwanza kubwa la mchezo huo jijini New York mwaka uliopita chini ya usimamizi wa Gilbert.
SOMA: Fahamu mashindano makubwa ya tenisi duniani
Lakini amelipoteza mwaka huu katika raundi ya nne kwa Mmarekani mwenzake Emma Navarro.
Gauff alimuajiri Gilbert Julai 20, 2023 kufanya kazi pamoja na kocha wa kihispania Pere Riba baada ya kutolewa raundi ya kwanza ya michuano ya Wimbledon mwaka uliopita.



