CONGO: Zaidi ya watu 170 wahukumiwa kifo

CONGO : SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Felix Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu kadhaa waliopatikana na hatia ya kushiriki kwenye magenge ya wahalifu.

Shirika hilo limenukuu ripoti zinazoeleza kwamba zaidi ya watu 170 wamepangwa kunyongwa nchini humo.

Mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Sarah Jackson amezitaja taarifa hizo za watu kunyongwa kuwa za kushtua. SOMA: DRC Congo na Rwanda kumaliza mapigano

Advertisement

Mamlaka nchini Congo zimewahukumu mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa magenge ya wahalifu, wanaojulikana kama kulunas, kama sehemu ya oparesheni kubwa dhidi ya magenge ya wahalifu.

Wengi wao wanakabiliwa na hukumu ya kifo kwa makosa ya kufanya uhalifu kwenye maeneo ya mijini na wanashikiliwa katika magereza yenye ulinzi mkali.