COP30 iwe muarobaini wa ukame, mafuriko EAC

NOVEMBA mwaka huu dunia itakutana nchini Brazil kwenye Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UNFCCC) kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP30).
Mkutano huo, moja ya malengo yake ni kuiepusha dunia na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuweka mikakati ya kupambana nazo kuifanya kuwa sehemu salama ya kuishi.
Uhalisia ulivyo kwa sasa, Afrika Mashariki inakabiliwa na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame, mafuriko na uhaba wa chakula.
Hivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inahitaji ujumbe wa pamoja ulioratibiwa vizuri kutafuta na kuja na majibu ya namna ya kuondokana na kadhia hiyo.
SOMA: Nchi za EAC zijipange kukabili joto, ukame
Ni wazi kuwa COP30 inaweza kuitoa kanda kutoka kwenye ukame na njaa na kuwa yenye neema na chakula cha kutosha kiasi cha kusaidia kanda nyingine.
Takwimu zinaonesha kuwa Somalia, Sudan Kusini na Kenya zimekuwa zikikumbwa na ukame hatari unaosababisha njaa kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha.
Wakati nchi hizo mambo yakiwa namna hiyo, mambo ni tofauti kwa Tanzania, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi kwani zenyewe huathiriwa na mvua kubwa.
Mfano ni mwaka jana ambao kutokana na mvua za El nino, yalitokea mafuriko makubwa Rwanda, Uganda na baadhi ya maeneo ya Kenya.
Sote tunaamini kuwa hizo ni matokeo ya mabadiliko ya tabianchi. Ina maana mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ukosefu wa mvua na pia kupata mvua nyingi.
Tunaunga mkono ushiriki kikamilifu wa Sekretarieti ya EAC tukiamini ni kisemeo cha jumuiya hii kubwa Afrika inayoundwa na nchi nane.
Matarajio yetu ni kuwa ushiriki wa nchi hizi katika mkutano, utazaa matunda kwa kiwango kikubwa hali itakayofikisha mwisho matatizo ya ukosefu wa mvua na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa kupita kiasi kwa baadhi ya majira.
Sekretarieti imethibitisha dhamira yake ya kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama na wadau ili kuhakikisha kuwa sera hiyo inatekelezeka na inajibu changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika ukanda.
Tunazisihi nchi wanachana wa EAC kufuatilia kitakachoendelea Brazil kwa lengo la kujifunza na pia kuweka mipango ya utekelezaji wa maazimio yote yatakayofikiwa.
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern………………. http://Www.Cash43.Com
Earn extra cash every week from the comfort of your home! This flexible part-time opportunity is perfect for anyone looking to make 300-1300 Dollars weekly. Start now and receive your first payment in just a few days. Don’t miss out—join today. Tap on Finance Economy OR Investing..
Here’s what I do……………….. http://Www.Cashprofit7.site
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month.details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..
Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com