CSR| Usimamizi wa PURA waendelea kuzaa matunda kwa jamii

LINDI: Juhudi zinazowekwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) katika kusimamia masuala mbalimbali ikiwemo uwajibikaji wa kampuni kwa Jamii (CSR) zimeendelea kuzaa matunda na kuleta matokeo chanya katika jamii hususani zinazozunguka rasilimali za gesi na mafuta.

Kupitia miongozo, maelekezo na usimamizi wa PURA, kampuni zinazofanya shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini sasa zinashiriki kikamilifu katika masuala ya CSR.

Kupitia sera ya CSR, vijana 23 kutoka mkoa wa Lindi wampata udhamini kutoka kampuni za Equinor Tanzania na Shell Exploration and Production Tanzania Ltd kwa mwaka 2024/25 uliowazewesha kusoma na hatimaye kuhitimu mafunzo ya fani mbalim,bali zitolewazo na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ngazi ya tatu.

Vijana hao wamepata fursa ya kusomea fani mbalimbali zikiwemo umeme, ubunifu wa mavazi na teknolojia ya nguo, uchomeleaji na uungaji vyuma, viyoyozi na majokofu, ufundi magari na uashi.

Kupitia programu hiyo, iliyoanza mwaka 2022/2023, inafanya idadi ya wanufaika na wahitimu kufikia 71.

SOMA: DC Lindi: “Jitihada hazijawahi kumtupa mtu” 

Kampuni hizo pia zimewezesha vitendea kazi vya kuanzia kwa vijana waliohitimu kama njia ya kuwasaidia kutumia ujuzi walioupata kujiajiri.

Mahafali ya kuwatunuku wahitimu vyeti na kuwakabidhi vifaa yalifanyika Juni 10, 2025 katika Chuo cha VETA Lindi na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, kama mgeni rasmi.

Pamoja na kupongeza kampuni za Equinor na Shell kwa ufadhili huo, DC Mwanziva aliipongeza PURA kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii zinazoishi au kuzunguka maeneo ya utafutaji na uzalishaji wa gesi zinanufaika kutokana na shughuli hizo.

Mwanziva amewataka pia vijana wa Lindi kuchangamkia fursa ya udhadili uliotangazwa na Equinor na Shell Tanzania kwa mwaka 2025/26 ambapo mwisho kuomba ufadhili huo ni Juni 13, 2025.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button