CWT wanawake wasaidia vyakula wanafunzi Arusha

KAMATI ya Kitengo cha Walimu Wanawake Taifa kutoka Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kimetoa msaada wa taulo za kike, sukari kwa ajili ya walimu, mchele, sabuni na hela za kalamu kwa wanafunzi wa shule tatu zilizopo mkoani Arusha.
Zoezi la kukabithi vifaa hivyo katika shuleya Sekondari Arusha Girls, Shule ya Msingi Ilboru na Shule ya Msingi Meru kitengo maalum ili ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Taifa, Neema Obeidi amesema msaada huo umeenda sambamba na kuadhimisha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kitaifa Arusha.
“Thamani ya mtoto wa kike ni kubwa hivyo someni mtimize ndoto zenu ikiwemo kutunza utu wenu ili mtimize ndoto zenu, msikubali kurubuniwa someni haya mambo ya utandawazi mtakutana nayo badae”
Naye Ofisa Elimu Watu Wazima Idara ya Sekondari ,Charles Mwita ametoa namba ya simu ya mkononi kwa wanafunzi hap ili pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili au viashiria vinavyopelekea kushindwa kutumiza ndoto zao waripoti ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Wakati huo huo, Dada Mkuu wa shule ya Arusha Girls, Margeth Mollel ameshukuru kwa msaada huo alisisitiza katika maadhimisho ya wiki ya wanawake wasisahau pia watoto wakie ambao ni baba bora badae wasaidie kuhakikisha wanathamini watoto wakike ikiwemo kuwapa nafasi watoto wakike na kiume ili wawe wababa bora badae na kuwapa nafasi wanawake kujiendeleza zaidi.


