D Voice: Bado najitafuta nifike anga za kimataita
MSANII wa muziki wa singeli kutoka kundi la WCB Wasafi, Dvoice Ginni maarufu D Voice amesema bado anajitafuta ili afikie anga za kimataifa kama walivyo wasanii wa kundi hilo.
D Voice anayetamba na nyimbo nyingi ukiwemo wa ‘Kuachana Shingapi’ na ‘Madanga ya Mke Wangu’ amesema wasanii wengi wanaridhika wakiona wanakubalika katika baadhi ya mitaa wanaamini wamefanikiwa kisanii wakati bado.
“Wasanii wengi wakiona wanakubalika baadhi ya mitaa wanaamini wamemaliza wanaridhika mimi naona bado najitafuta kuelekea mafanikio ya kufanya shoo kubwa za kimataifa kama wanavyofanya wasanii wengine Mboso na bosi wangu Diamond,” amesema D Voice.
D Voice amesema kuwa WCB itasaidia kunyanyua muziki wa singeli huku akiamini kwamba muziki wa singeli unakwenda kupata heshima kubwa.
“Naamini mimi kuwa WCB kutabadilisha fikra ya muziki wa singeli kupitia mimi unakwenda kututambulisha kimataifa na mafanikio pia,” amesema D Voice.