DADA wa kazi aliye fahamika kwa jina moja la Neema (35) anatuhumiwa kutoweka kus ikojulikana na watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu na minne kutoka nyumbani kwa mwajiri wake, Hawa Suleiman.
Watoto hao ni Mahad Mohammad (4) na Husna Gu lam (3) ambao wametoweka nyumbani kwao maeneo ya Bandari wilayani Temeke, Dar es Salaam, juzi saa 12 jioni.
Akizungumza na HabariLEO jana, mama wa Mahad, Hawa alisema Neema ana siku nne tangu kufika nyumbani hapo kwa ajili ya kumsaidia kazi mbalimbali akitokea Kigoma. Husna ni mtoto wa kaka yake Hawa ambaye anamlea nyumbani kwake.
Alisema upatikanaji wa dada huyo ni kupitia kwa mfanyakazi wake wa awali, Salma Said ambaye walikaa naye kwa takribani mwaka mmoja.
Alieleza hivi karibuni dadhuyo aliomba likizo kwenda nyumbani kwao kuona wa zazi wake kwa kuwa amekaa muda mrefu na kwamba walikubaliana kuwa atarudi.
“Alipoondoka alichukua nguo nyingi, nilimuuliza kama atarudi akanijibu atarudi na kama kuna mabadiliko atanijulisha.
“Baada ya siku mbili tatu nilimpigia akawa hapatikani na nilipompigia baba yake kijijini alisema hawajamuona nyumbani,” alisema Hawa.
Alifafanua: “Kwa kuwa nilikuwa na shida, ilinibidi nitafute mfanyakazi mwingine wa kunisaidia dukani kabla yeye hajaondoka, aliniunganisha na msichana mwingine nilimtumia hadi nauli lakini hakuja.
“Lakini, nikapigiwa simu na mtu mwingine akaniambia kuwa namba yangu amepewa na msichana wangu wa awali.” Alieleza kuwa baada ya kuelezwa hivyo, alimkubalia na kupanga siku ya kuja kwani alidai kwamba anatokea Kigoma, hivyo alimtumia nauli.
Hawa alisema alipofika dada huyo, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani na kuzungumza na simu na kwamba alikuwa akitoka nje pindi atakapoagizwa kufanya kazi fulani.
Pia, alisema siku ya ku potea kwa watoto hao, yeye aliondoka nyumbani na kuwaacha dada, watoto pamoja na mama yake mzazi.
“Wakati mama ameingia kuswali jioni, ndipo dada ali toka na watoto hawa na baada ya mama kumaliza kuswali alinipigia simu akanijulisha kuwa dada ameondoka na watoto na hajarudi mpaka sasa. Wakati huo huo nilim pigia lakini hakupatikana,” alisisitiza.
Baba wa Mahad, Mohammad Kassim alisema kuwa dada huyo aliondoka na mtoto saa 12:00 jioni na walipomtafuta katika simu yake haikupatikana.
Alisema mzazi mwenzake (Hawa) ndiye anayeishi na mtoto huyo na yeye anahusika na malezi na kwamba aliwahi kujulishwa kuhusu kutafuta dada wa kazi baada ya ali yekuwa naye awali kuondoka.
“Alifanyiwa mpango wa kupata dada mwingine wa kumsaidia na mtu tu na hai kuwa kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika. Ilikuwa ni connection (kuunganishiwa) aliambiwa tuma nauli, tulituma, dada akadai amepanda basi na amefika kituoni, wakaenda kumchukua kwenda nyumbani,” alisema Kassim.
Alisema siku ya tukio mmoja wa marafiki zake walimuomba namba ya dada huyo (Neema) na kuifuatilia ambapo mara ya mwisho alionekana maeneo ya Shule ya Wailes na wakati huohuo alizima simu yake.
“Tunaomba mtusaidie kwa watakaowaona mmoja mmoja au wote mtoe taarifa polisi au kwa kupiga simu 0744555574,” alisema Kassim.
Hata hivyo, alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, John Malulu alisema kuwa mtoa taarifa kuhusu tukio hilo ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambaye pia simu zake hazikupokelewa.