Dakika 120 za kurekebisha maumbo ya wanawake 4 Muhimbili-Mloganzila

Mtu wa tano ambaye ni mwanaume 'aghairi'

DAR ES SALAAM: JOPO la madaktari limetumia jumla ya saa mbili kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha  maumbo ya wanawake wanne kwa lengo la kupunguza uzito katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mwanaume mmoja aliyekuwa kwenye orodha hiyo hakuonekana leo, Oktoba 28, 2023, ikiwa ndiyo siku ambayo hospitali imeanza kutoa huduma hiyo kwa mara ya kwanza nchini.

Akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam baada ya zoezi hilo kufanyika, Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali hiyo, Dk Erick Muhumba amesema kutokana na hali zao kuendelea vizuri, wanawake hao wanatarajiwa kuruhusiwa kutoka wodini kesho, Jumapili.

Hii ni mara ya kwanza kwa hospitali ya Tanzania kufanya upasuaji wa kurekebisha maumbo katika zililowahusisha madaktari wazawa zaidi ya 10 kwa daktari bingwa wa upasuaji kutoka India.

Kwa mujibu wa Dk Erick Muhumba, upasuaji huo ulichukua dakika 20 kwa kila mgongwa.

Hata hivyo, pamoja na maandalizi mengine, Hospitali hiyo ilifanikiwa kumaliza zoezi ndani ya saa mbili.

“Upasuaji umefanikiwa vizuri kabisa na wagonjwa wako wodi hao wote hali zao zinaeneelea vizuri kwa mtu mmoja … tutawaruhusu kesho,” ameongeza.

 

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button