Daraja Kitengule lakamilika kwa asilimia 99

UJENZI wa daraja la Kitengule kwenye mto Kagera uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 31 .5 umekamilika kwa asilimia 99 likiwa na urefu wa mita 140 lililopo Wilaya ya Misenyi, Kagera.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Kagera, mhandisi Ntuli Mwaikokesya amesema hayo Novemba 11, 2023 alipozungumza na waandishi wa habari Kanda ya Ziwa waliotembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na serikali.

Mhandisi Mwaikokesya alisema zaidi ya sh bilioni 26 zilizotolewa na serikali zimekamilisha ujenzi huo ambapo kiwanda cha sukari Kagera (Kagera sugar LTD) kimetoa Sh Bilioni 5 na ardhi iliyojengwa daraja na barabara kiwango cha lami chenye urefu wa kilomita 18.

Mhandisi Mwaikokesya alisema daraja kwa litaunganisha barabara mbili za Kakunyu kwenda Kiwandani Kagera sugar,Kyaka kwenda Bugene hadi Kasulo kwa lengo la kuunganisha Wilaya za Misenyi na Karagwe.

“Mradi huu unamanufaa mahususi ya kufupisha umbali wa kilomita 28 wa usafirishaji wa Mali ghafi (miwa) kutoka shabani na kwenda kwenye kiwanda cha sukari kilichopo wilaya ya Misenyi” alisema Mhandisi Mwaikokesya.

Mhandisi Mwaikokesya alisema daraja hilo limeweza kuwaunganisha wakazi wa wilaya mbili ambapo upande wa Wilaya ya Karagwe kuna mashamba mapya yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 16,000 yanayomilikiwa na kiwanda pamoja na wakulima wadogowadogo.

Mhandisi Mwaikokesya alisema daraja pia limepunguza mzunguko badala ya kupitia daraja la Kyaka kupeleka malighafi sasa linapitia daraja Kitengule na kupunguza malori kwenye makutano ya njia ya Kyaka.

Mhandisi Mshauri Mohamood Kitime kutoka kampuni ya Lukutani na Wahandisi alisema daraja hilo wamejenga linauwezo wa kudumu miaka 50 na kupitisha mzigo wenye tani 100 hivyo wananchi wanatakiwa kulitunza.

Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Misenyi mchungaji Enock Bona na philibert Fideli walisema wanaipongeza serikali kujenga daraja hilo kwani walikuwa wakitumia muda mrefu kuzunguka sababu hakukuwa na daraja na sasa lipo wanawahi kwenye majukumu yao.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button