DC ataka viongozi wa dini washirikishwe lishe bora

TANGA; Kilindi. Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa amewataka wataalamu wa lishe kushirikiana na viongozi wakiwemo wa dini katika kuelimisha jamii kuzingatia lishe bora ili kuepukana na changamoto za afya zinazotokana na ulaji usiofaa pamoja na kutofanya mazoezi.

Hayo ameyasema wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu kilichofanyika wilayani huo.

Amesema kuwa magonjwa na matatizo mengi ya kiafya yanasababishwa na ulaji usiozingatia makundi ya vyakula, kama ambavyo wataalamu wa lishe wamekuwa wakielekeza.

“Pelekeni hii elimu ya lishe katika ngazi za jamii shirikisheni viongozi wa dini, ili elimu hii iweze kuwafikia watu wengi na kubadili tabia zao za lishe, ili kupunguza changamoto ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na lishe mbaya,”amesema mkuu huyo wa wilaya.

Amesema kuwa jamii inahitaji kujifunza kwa vizazi vilivyopita, vilikuwa havisumbuliwi na magonjwa kama ilivyobsasa kwabsababu walikuwa wanakula vyakula vya asili na kufanyakazi za nguvu, ambazo ni  mazoezi tosha.

Awali akiwasilisha taarifa ya mkataba wa lishe, ofisa lishe wa wilaya hiyo Philimon  Nsodya amesema kuwa robo ya Julai na Septemba kiashiria namba 1 kuhusu shule za msingi na sekondari zinazotoa chakula cha mchana kimefanya vizuri, kwani katika kata 15 wamepata alama ya kijani kwa kutoa chakula kwa zaidi ya asilimia 72.6.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button