DC Mahawe afariki dunia, Rais Samia aomboleza

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Ester Mahawe.

MKUU wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Ester Mahawe amefariki dunia leo mkoani Kilimanjaro.

Taarifa ya kifo cha DC Mahawe imetolewa mkoani Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa.

Kufuatia kifo hicho Rais Dk Samia Suluhu Hassan ametuma salama za rambirambi akisema: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.”

Advertisement

Rais Samia ametoa pole kwa familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji,”amesema Rais Samia.