DC Mgandilwa apiga kura

MKUU wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa ameungana na wananchi wenzake wa mtaa wa Legeza Mwendo kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo.

DC Mgandalwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kuchangua viongozi waadilifu ambao wataweza kushirikina nao katika kuwaletea maendeleo.

Advertisement

“Niwaombe wananchi twende tukachagua viongozi ambao wataweza kutuletea maendeleo lakini na kusimamia Kwa ukaribu utekelezaji wa miradi,” amesema.