SINGIDA: MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dk Fatma Mganga wamefanya ziara kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari.
Ziara iliyofanyika Januari 17, 2025, DC Mwenda amewaagiza wataalamu wanaosimamia miradi hiyo kufanya kazi kwa uharaka na uadilifu ili kukamilisha miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
“Lazima tuhakikishe tunakwenda na kasi ili tuendane na muda miradi iishe kwa wakati ili wanafunzi waweze kuanza masomo yao kwa wakati na tuisimamie kwa uadilifu na ubora unaotakiwa,” amesema DC Mwenda.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dk Fatuma Mganga ametoa wito kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ufaulu zaidi katika Mkoa wa Singida huku akipongeza ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa Shule ya Msingi Tyeme.