Dhamira za kisiasa zinusuru mito isikauke
KWA kipindi cha Novemba 10 hadi 15 mwaka 2025 na kwa neema ya Mungu, nilitembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha (RUNAPA) mkoani Iringa, Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania.
Hifadhi hiyo ni moja ya hifadhi za taifa katika Ukanda wa Kusini wenye rasilimali muhimu za kuvutia watalii wa ndani na wa kutoka nje ya nchi. Mbali na Runapa, zipo pia hifadhi nyingine zenye utajiri wa wanyamapori mathalani, hifadhi za Kitulo, Mikumi, Nyerere na Udzungwa.
Hifadhi hizi pamoja na magofu ya kihistoria yaliyopo Kilwa-Masoko, zikiunganishwa kwa pamoja ni rasilimali muhimu kuendeleza utalii Kusini mwa Tanzania. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika Runapa na kutathmini kwa haraka ili kubaini hali halisi ya ikolojia ilivyo katika hifadhi wakati wa kiangazi.
Kwa ushirikiano na watumishi wa hifadhi, nilijionea uhalisia, hasa katika maeneo ya Ihefu na Usangu. Maeneo hayo ni yenye ardhi oevu ambayo ni muhimu kwa uhifadhi wa maji ambayo ni chanzo muhimu cha maji yanayotiririka katika Mto Ruaha-Mkuu na mkondo wake kupita eneo la hifadhi hadi mabwawa ya kuzalisha umeme, Mtera na Kidatu na hatimaye, Bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji.
Nilipigwa na butwaa kushuhudia kuwa mkondo wa maji wa Mto Ruaha Mkuu, hauna maji yanayotiririka. Hii ina maana kwamba, yamekauka isipokuwa niliona sehemu chache zikiwa na maji kidogo sana. Mara ya kwanza nilipotembelea Hifadhi Ruaha mwaka 2018, hali ya mazingira kwenye ardhi oevu ya Usangu na Ihefu haikuwa ya kutisha kama hali halisi ilivyo mwaka 2025.

Kadhalika, ziara ya 2018 ilikuwa wakati wa kiangazi lakini kwa kiasi fulani, maji yalikuwepo kwenye ardhi oevu Usangu na mengi zaidi katika eneo la Ihefu. Wakati ule, mimea hasa nyasi ndefu pamoja na aina nyingine za mimea asilia ilionekana ikistawi na Ihefu ilikuwa na maji ya kutosha, kufanya Mto Ruaha Mkuu uendelee kutiririsha maji katika mkondo wake.
Kwa kutumia mashua, iliwezekana kufikia maeneo kadhaa bila kwenda umbali mferu kutokana na uwepo wa viboko na mamba. Uzoefu unaonesha kuwa, kupungua kiwango cha maji eneo la Ihefu ilianza kujitokeza 2021 na tangu wakati huo, uhaba wa maji ukawa ukiongezeka, kiasi cha kuhatarisha uhai wa wanyamapori hifadhini.
Nilichokishuhudia Novemba mwaka 2025 ni hali inayotisha, maana sikuona maji mengi kwenye eneo ardhi oevu Usangu na Ihefu. Ilibainika kuwa, eneo kubwa lilikuwa kavu na nyasi zimechomwa moto. Ihefu ni sehemu muhimu ya ardhi oevu ndani ya uwanda wa Usangu lakini sasa eneo hilo limekauka maji na kuathiri mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu.
Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa, kuongezeka kwa shughuli za binadamu, hususan matumizi ya maji mengi kwa kilimo cha mpunga, kumesababisha maji kupungua sana kwenye ardhi oevu katika uwanda wa Usangu na Ihefu. Uzoefu unaonesha kuwa, maji yanachepushwa kutoka kwenye mito na hali imekuwa hivyo zaidi ya miongo minne iliyopita.
Mbali na wakulima wenye maeneo madogo, kuna zaidi ya hekta 45,000 zinazoendeshwa na wakulima wakubwa wanaotumia maji mengi, hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa utiririshaji maji kwenye Mto Ruaha Mkuu. Kadhalika, kuongezeka shughuli za binadamu zisizo endelevu katika maeneo ya miinuko kumekuwa chanzo cha mmomonyoko wa udongo ambao husafirishwa na maji ya mvua hadi kwenye mito na mabonde.
Kwa mantiki hiyo, uwezo wa kuhifadhi maji mengi katika eneo la Ihefu umekuwa ukipungua kila mwaka kutokana na udongo/ mchanga kujaa kwenye ardhi oevu nyakati za mvua (Masika). Hali hiyo imeendelea kwa muda mrefu, hivyo kusababisha maji kukauka haraka hususan katika majira ya kiangazi mwaka 2025.
Vivyohivyo, athari hasi pia zinaonekana kwenye mkondo wa Mto Ruaha Mkuu, zikiwa ni pamoja na mto kukauka na wanyamapori kukosa maji. Hali hiyo inadhihirika Novemba 12, 2025 tulipotembelea sehemu kadhaa kujionea hali halisi katika Mto Ruaha Mkuu ndani ya hifadhi hiyo.
Mto huo ulikuwa mkavu, kiasi cha gari kuvuka mto mara mbili bila tatizo. Kadhalika, katika mkondo wa mto, nilichokiona ni udongo/ mchanga mwingi na kwenye maeneo kadhaa, mawe/ changarawe vilidhihirika waziwazi. Hata-hivyo, ni kiasi kidogo cha maji kwenye madimbwi mawili ambamo viboko wengi walikuwa wamebanana humo ili kuishi.
Nilitaarifiwa kuwa sehemu hizo zenye maji ni matokeo chanya ya juhudi za watumishi hifadhini kujitahidi kufukua na kuondoa mchanga/ udongo, mpaka walipofikia sehemu yenye maji na kutengeneza madimbwi kunusuru maisha ya viboko na mamba.
Kukosekana maji ndani ya hifadhi ni changamoto kubwa, kwa sababu baadhi ya wanyamapori kwa mfano, tembo wanatumia ‘meno’ pia kuchimba mchanga/ udongo kupata maji. Katika maeneo fulani ndani ya hifadhi, tembo wanaharibu miti kama mibuyu na aina ya migunga ili kupata sehemu za ndani ya mti ambazo ni laini na zenye majimaji kupunguza kiu.
Kimsingi, umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza mazingira-rafiki katika ardhi oevu Ihefu na Usangu kwa ujumla, ni suala linalopasa kupewa msukumo wa juu. Hii ni pamoja na kuhamasisha utashi na msukumo kisiasa, kutokana na unyeti wa maeneo hayo ili kurejesha mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu nyakati za Masika na Kiangazi.
Uwepo wa dhamira thabiti kisiasa utapunguza changamoto zilizosababisha mto kukauka. Uzoefu unaonesha sehemu ya Mashariki ambako kuna ardhi oevu ya Ihefu, vyanzo vyake vya maji ni maeneo ya milimani katika Ukanda wa Juu ambako sehemu asilimia 60 ni mkoani Mbeya na asilimia 40 katika maeneo ya Iringa na Njombe.
Huko kuna makazi ya watu, pia kuna misitu na maeneo muhimu ya kuhifadhi vyanzo ya maji. Mito inayoingiza maji kwenye ardhi oevu Usangu ni Chimala, Kimani, Mbarali, Mkoji, Ndembera na Ruaha ambayo vyanzo vyake ni sehemu za juu milimani, pia kupelekea ardhi oevu eneo la Ihefu kuwa chimbuko la Mto Ruaha Mkuu.
Tanzania ni taifa linalokua kiuchumi hadi kufikia kipato cha kati, hivyo ni wakati wa kupata suluhisho la haraka ili maji katika Mto Ruaha- Mkuu yaendelee kutiririka mwaka mzima, bila kuathiri masuala muhimu ya kiuchumi na kijamii.
Kutokana na hali hiyo, ni vema kutafuta suluhisho la kudumu kupitia juhudi za pamoja kitaifa ili matokeo chanya yapatikane haraka. Kwa msingi huo, ni muhimu mamlaka za juu kitaifa katika Serikali Kuu na serikali za mitaa pamoja na watunga sera na wafanya uamuzi kuweka mikakati ya kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa, vinatunzwa na kulindwa ipasavyo.
Kadhalika, mito muhimu kama Ruaha-Mkuu, Ruaha Mdogo, Mara, Kilombero, Rufuji, Kihansi, Pangani, Wami, Kagera, Ruvuma, Zigi, Malagalasi na mingineyo nchini itazamwe kwa umakini zaidi, tangu inapoanzia hadi kwenye mabwawa, maziwa au baharini na kuhakikisha inalindwa kwa manufaa ya umma.
Sheria zilizopo, mfano kuzuia shughuli za kibinadamu kuanzia kingo za mito hadi meta 30 au 60 kulingana na
ukubwa wa mto, zitekelezwe na kusimamiwa ipasavyo.




6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO
Mpango Elekezi 2050 umeainisha miradi 14 ya kielelezo. Miradi hii inalenga kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa kijani. Itasaidia kukuza nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ya kisasa. Aidha, miradi hii inalenga kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa. Miradi hiyo imepangwa kama ifuatavyo:
NO PROGRAMME
1 Mageuzi ya Viwanda kwa Ukuaji wa Uchumi
2 Ujumuishaji wa Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi wa Kijani
3 Ubunifu wa Kidijitali na Miundombinu Mahiri kwa Ukuaji wa Siku za Usoni
4 Ujenzi wa Uhimilivu wa Tabianchi na Uchumi Endelevu wa Kijani
5 Kuendeleza Miundombinu na Muunganisho wa Usafiri kwa Tanzania kuwa Kitovu cha Kikanda
6 Mageuzi ya Sekta ya Nishati kwa Umeme Safi na Endelevu
7 Kukuza nguvukazi yenye Afya, Elimu na Ujuzi
8 Kuimarisha Utawala Bora, Uwajibikaji na Mifumo ya Udhibiti
9 Kuendeleza Miji Mahiri na Miundombinu Endelevu ya Mijini
10 Kuchochea Biashara, Uwekezaji na Upanuzi wa Uchumi
11 Kupanua Sekta ya Utalii na Uchumi wa Utamaduni
12 Kubadilisha Sekta ya Kilimo na Uchumi wa Vijijini
13 Kuboresha Elimu, Utafiti na Ubunifu wa Kiteknolojia
14 Mageuzi ya Kifedha ya Kidijitali na Jumuishi