Diamond aongoza kupokea mkwanja mrefu
WASANII wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ Raymond Shaban ‘Rayvanny’ na Rajab Abdul ‘Harmonize’ wametajwa kuwa wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye onesho moja.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa jarida la Afrika la African Fact Zone.
Katika orodha hiyo Diamond Platnumz analipwa Sh milioni 250, Ali Kiba Sh milioni 100.
Harmonize anafuatia akilipwa Sh milioni 50 huku Rayvanny akilipwa Sh milioni 40.
Katika Jarida hilo limewataja pia wakali kutoka nchini Nigeria ambao Burna Boy, Wizkid, Rema kama vinara wa kulipwa pesa ndefu zaidi, wakali hao wanapokea Dola milioni moja ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.
5.