MAREKANI : RAPA maarufu wa hip pop nchini Marekani Sean Diddy Combs anakabiliwa na mashataka mapya ya kuwadhalilisha wavulana wawili katika nyakati tofauti huko nchini Marekani .
Kesi hizo zimewasilishwa wakati wa muendelezo wa kesi yake ya udhalilishaji wa kingono inayoendelea nchini Marekani.
Katika kesi ya kwanza iliyowasilishwa,Sean Diddy anadaiwa kumvamia kijana mmoja na kumpiga katika chumba cha hoteli huko New york mwaka 2005.
Wakati akimpiga kijana huyo anadaiwa kumpa dawa za kulevya kwa nguvu na kumdhalilisha kingono mvulana huyo ambaye alikuwa ana miaka 10 .
Kesi ya pili, Sean Diddy alimshambulia kijana mwingine mwenye umri wa miaka 17 ambaye alishiriki katika kipindi cha televisheni cha Making the Band mwaka wa 2008.
Hatahivyo , wanasheria wanaomtetea Sean Diddy wamesema mashtaka hayo hayana ukweli wowote wa kuthibitisha.