RASIMU ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeeleza kuwa in[1]aongozwa na misingi sita, ikiwamo umoja na kwamba kila Mtanzania ana jukumu la kudumisha Muungano, umoja na mshikamano wa kitaifa. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alizindua rasimu hiyo Unguja juzi na akasema imebeba matamanio ya kila Mtanzania na itakuwa na ma[1]lengo makuu matano.
Rasimu hiyo imetaja msingi wake wa pili ni utu kwamba kila mtu anas[1]tahili kuheshimiwa, kuthaminiwa na kulindiwa utu wake. Msingi wa tatu wa rasimu hiyo ni haki za binadamu, hivyo kila mtu ana haki ya kufurahia uhuru na kulindwa kwa mujibu wa Katiba.
Imetaja msingi wake wa nne ni demokrasia kwa sababu kila mtu, jamii na taifa kwa ujumla linaheshimu na kuzingatia Katiba, mgawanyo wa mamlaka, uhuru wa mahakama, ku[1]wepo kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, utawala wa sheria na ushiriki sawa wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwenye michakato ya uamuzi.
Kuhusu ulinzi wa maliasili na rasilimali ambao ni msingi wa tano imeeleza kuwa maliasili na rasilimali za Tanzania ni vitu vyenye thamani kubwa kwa watu wake. hivyo, zinapaswa kusimamiwa, kulindwa na kutumiwa vyema kwa maendeleo endelevu na ustawi wa taifa na kwa manufaa ya kizazi cha leo na vizazi vijavyo.
Katika msingi wa sita ambao ni ulinzi wa utamaduni na maadili ya Taifa, dira imeeleza kuwa urithi wa utamaduni wa Tanzania na maadili ya taifa vitahifadhiwa, vitakuzwa na kulindwa ili kujenga utambulisho wa kitaifa na umoja na kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Tanzania ya mwaka 2050 Aidha, rasimu hiyo imeeleza kuwa ifikapo 2050, Tanzania inatarajiwa kuwa Taifa lenye maendeleo yanayolingana na nchi zenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu au zaidi. Imeeleza kuwa ili kufikia hatua hiyo yanahitajika mageuzi kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 140 na kwamba zaidi ya nusu watakuwa wa[1]naishi mijini na inatarajiwa wengi wao watakuwa ni vijana.
Rasimu hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo litakuwa na athari katika uhakika wa chakula, ukuaji wa miji, fursa za ajira na upatikanaji wa huduma za elimu na afya. Hata hivyo, imesema uwekezaji wa kimkakati katika sekta muhimu kama vile kilimo, madini, utalii, uzalishaji viwandani na teknolojia utawezesha uchumi kukua kwa takribani mara nne ya kiwango cha sasa.
Rasimu imesema Tanzania kuele[1]kea 2050 inajiandaa kukabili changa[1]moto zinazotarajiwa kutokea duniani, ikiwamo ya kuvurugika kwa mfumo unaoongozwa na kanuni za kimataifa kwa sababu jambo hilo linaweza kuwa tishio kwa jitihada za Tanzania za kujile[1]tea maendeleo.
Pia, inajiandaa kukabiliana na mab[1]adiliko ya nguvu za kiuchumi na kisiasa za mataifa makubwa, kukosekana kwa usawa, ukuaji wa miji, mabadiliko ya ta[1]bia ya nchi na ya kidemografia, mageuzi ya kiteknolojia na mivutano ya kisiasa. Aidha, imeeleza kuwa kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea duniani, Dira 2050 inalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye nguvu kiuchumi Afrika na duniani kwa ujumla na kuwa taifa imara linaloweza kukabili changamoto zinazotokana na mabadiliko duniani.