Dissanayaka aapishwa urais

SRI LANKA : RAIS mteule Anura Kumara Dissanayaka ameapishwa leo nchini  Sri Lanka, baaada ya kushinda kwa zaidi ya kura milioni 1.3  dhdi ya mpinzani wake .

Kiongozi huyo ambaye anafuata siasa za Kimarx na ambaye chama chake kiliongoza maandamano ya umma mara mbili yaliyopelekea vifo vya maelfu ya raia, alipata uungaji mkono mkubwa kufuatia hali ya kuporomoka kwa uchumi mwaka 2022.

Dissanayaka, mwenye umri wa miaka 55 anamrithi Rais Ranil Wickremesinghe, mwenye umri wa miaka 75, ambaye alichukuwa madaraka kufuatia mapinduzi nchini humo .

Wickremesinghe aliongoza kwa kuongeza kodi na hatua nyengine za kubana matumizi akifuata masharti ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.

SOMA : BUNGE LA SRI LANKA LATOA MWEZI MMOJA KUMPATA RAIS MPYA

Ingawa alifanikiwa kuondosha upungufu wa huduma muhimu na kujikita zaidi katika kukuza  uchumi katika nchi hiyo lakini bado  hali ya maisha ya raia nchini  humo yalikuwa  katika hali ya ufukara .

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button