Dk.Biteko aitaka TANESCO kumaliza kero ya Umeme
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.
Dotto Biteko amelitaka shirika la umeme Tanzania TANESCO kushughulikia adha ya umeme iliyopo kwa sasa nchini.
Aidha Dk, Biteko amewataka TANESCO kutohudhuria Kongamano la Nishati linalofanyika Dar es Salaam katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere ili wapambane na tatizo hilo la upungufu wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.
Dk Biteko ameeleza hayo wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufungua kongamano hilo.