Dk Biteko akagua ujenzi wa Majengo ya Wizara Mtumba

DODOMA: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Dk. Biteko  aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.

Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dk. Biteko ameshuhudia ujenzi ukiendelea ambapo kwa sasa umefikia asilimia 69 na Mkandarasi anayehusika na ujenzi huo ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.

 

Habari Zifananazo

Back to top button