MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Catumbela nchini Angola leo Desemba 04.
Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani, Kongo na Zambia kuhusu Ushoroba wa Lobito (Lobito Corridor), ambapo Tanzania ni mgeni mwalikwa katika Mkutano huo unaofanyika katika mji wa Lobito, Angola leo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)