Dk Mpango ataka vijana wakimbilie VETA

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango ametoa rai kwa vijana wakike na wakiume kwenda Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kusomea fani mbalimbali ikiwemo ufundi wa kushona nguo badala ya kuwaachia mafundi wanawake pekee

Dk, Mpango ametoa agizo hilo leo eneo la Samunge wilayani Ngorongoro wakati wa ufunguzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Ngorongoro, Arusha.

Amesema amejionea maendeleo makubwa yaliyofanywa na wanarika ya Irumeshari jamii ya Wasonjo ikiwemo katika juhudi kubwa za kimaendeleo hususan elimu ya mafunzo stadi

Ametoa rai kwa vijana wa kiume kujiunga na chuo hicho kwenye fani mbalimbali ikiwemo fani ya ushonaji kwani alipotembelea chuo hicho amewaona mvulana mmoja huku wasichana wakiwa wengi.

“vijana wakiume na wakike ingieni katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi ili mpate ujuzi mbalimbali kwani nimeona mvulana mmoja tu akiwa anashona”

Ameagiza Wakala wa Barabara Mkoa wa Arusha,kuhakikisha wanaitengeneza barabara hiyo ili iweze kupitika maji yote na kuagiza changamoto ya ukosefu wa maji itatuliwe haraka ili wananchi na wanafunzi wa chuo hicho waweze kupa maji safi na salama

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Anthony Kasore amesema chuo hicho kimefanikiwa kudahili wanafunzi 147 ambapo wasichana ni 68 na wavulana 79 katika faini ya umeme,ubunifu wa mavazi,ushonaji na Teknolojia ya nguo na uashi

Lakini pia miundombinu ya barabara inahitajika kwani barabara hiyo nyakati za mvua haipitiki na kupeleka ongezeko la gharama za usafiri sanjari na uhitaji wa Nyumba za watumishi pamoja na ukosefu wa uzio unaozunguuka chuo hicho unaopelekea uvamizi wa wanyana na wananchi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema eneo la Samunge ni maarufu sana kwani watu walikuwa wakienda kupata kikombe cha babu wa Loliondo.

pharmacy

Alisema Samunge ni eneo la kimaendelo kutokana na mfumo wao wa kimila kwa wanarikal la Irumeshari jamii ya Wasonjo kutoa mchango mkubwa wa kimaendelo na wanalima na kufuga pia

Habari Zifananazo

Back to top button