Dk Mpango atoa futari kwa yatima, wajane Kigoma

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango ametoa futari kwa wajane na yatima zaidi ya 300 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Futari hiyo imetolewa na shekhe wa Mkoa Kigoma, Hassan Kiburwa kwa niaba ya Makamu wa Rais ambapo Kiburwa amesema Dk Mpango amekabidhi futari hiyo kutimiza matakwa ya dini ya kuwasaidia wenye uhitaji.

Shekhe Kiburwa amsema imekuwa kawaida ya Makamu wa Rais kuwasaidia wenye uhitaji mkoani humo ikiwemo waumini wa kiislam na kwamba anafanya hivyo kwa mapenzi na ubinadamu wake bila kujali itikadi za dini.

Advertisement

Shekhe wa Mkoa Kigoma Hassan Kiburwa (kulia) akikabidhi futari kwa wanawake wajane wa Manispaa ya Kigoma Ujiji iliyotolewa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango

Pia walikabidhiwa mchele, sukari,unga wa ngano na maharage pia Jumapili jioni alitarajia kuwafuturisha watoto yatima zaidi ya 300 wanaohifadhiwa kwenye kituo cha Manara Ujiji mkoani Kigoma.

Baadhi ya wanawake wajane waliopokea futari hiyo akiwemo Moza Mohamed alimshukuru Makamu wa Raisi kwa msaada huo wa Futari kwa wanawake wajane mkoani Kigoma kwamba anaonyesha kujali hali za watu wa kipato cha chini bila kujali dini zao.

Moza Mohamed mmoja wa wanawake wajane alipokea futari iliyotolewa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwa wanawake wajane wa Kiislam Manispaa ya Kigoma kwa ajili ya mfungo wa Ramadhan.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *