Dk Muyungi akutana na Mkurugenzi wa Good Neighbors Tanzania

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Richard Muyungi (kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors Tanzania, Ilsun Jung ambalo limeonesha nia ya kuwekeza katika Biashara ya Kaboni.
Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam, leo Januari 23, 2026.

Amesema kwamba “Tanzania imekua ikishirikiana na Serikali ya Korea kwa muda mrefu hususani katika sekta ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na hivyo kuipongeza kwa kuendelea kutoa ushirikiano huo”.



