Dk Mwinyi apokea kitabu cha kampeni Uchaguzi Mkuu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amepokea Kitabu Maalumu chenye mkusanyiko wa habari picha za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar 2025.Kitabu hicho kimekabidhiwa jana na Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Benny Kisaka.

Akizungumza baada ya kupokea kitabu hicho, Rais Dk Mwinyi amempongeza Kisaka kwa ubora, umakini na weledi mkubwa uliotumika katika kuandaa na kukusanya taarifa zilizomo ndani ya kitabu hicho. Amesema kazi hiyo ni ya thamani katika kuhifadhi historia ya kampeni za uchaguzi Zanzibar zilizoanza Septemba 11 na kukamilika Oktoba 27, mwaka huu.

Naye Kisaka amesema kitabu hicho kitaanza kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa lengo la kufikisha taarifa hiyo kwa umma na kuhakikisha historia hiyo muhimu inabaki kumbukumbu ya vizazi vijavyo. SOMA: Vijana watakiwa kutumia hotuba ya rais kupata suluhu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button